• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Umaskini Kenya umefikia asilimia 29.2

    (GMT+08:00) 2018-10-18 20:26:53

    Benki ya dunia imeripoti kwamba viwango vya umaskini Kenya bado vipo juu .

    Kwa mujibu wa ripoti hii,wakenya milioni 14.2 ambayo ni asilimia 29.2 ya wakenya wanaishi kwa umaskini, huku wakikikosa hata uwezo wa kupata mambo ya msingi ya maisha.

    Ukosefu wa ajira umetajwa kuwa chanzo kikuu cha umaskini huo .

    Ripoti hiyo vile vile imeelezea ,licha ya umaskini huo unaokabili nchi nyingi duniani,shughuli za kiuchumi zilizoanza kuimarika hatimae zitapunguza umaskini.

    Watu wanaoishi sehemu za mashinani ndio wanaongoza kwa umaskini haswa vijana walio na umri wa chini ya miaka 18 ambao hawajapata elimu.

    Fauka ya hayo, azimio la Kenya kutaka kumaliza umaskini kufikia mwaka 2030 halitaafikiwa, kwani hadi sasa baadhi ya wakenya hawawezi kupata zaidi ya dola 1 nukta 5 kwa siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako