Katibu mtendaji wa Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa ECA Bibi Vera Songwe ametoa wito kwa nchi za Afrika kuichukulia kamati hiyo kama mshauri bingwa katika kukabiliana na changamoto za kijamii, kiuchumi na kimazingira.
Bibi Songwe amesisitiza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na masuala yanayofanana wakati changamoto za dunia zikizidi kuongezeka, na ametangaza uamuzi wa kamati yake kuhusu kushughulikia changamoto zinazozikabili nchi za Afrika.
Bibi Songwe pia amesema ECA inaweza kutoa ufumbuzi wa kuharakisha mchakato wa kutimiza Ajenda ya maendeleo ya 2063 ya Afrika, na malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya dunia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |