• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano wa vyombo vya habari wajenga daraja kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-10-19 18:46:48

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Habari la Zanzibar Bw. Muhammed Seif Khatib amesema, maendeleo ya kina ya ushirikiano wa vyombo vya habari vya China na Afrika yamejenga daraja kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.

    Bw. Khatib ameyasema hayo leo hapa Beijing alipohudhuria mkutano wa kamati ya Shirikisho la Vyombo vya Habari vya Video vya Afrika. Amesema shirika lake limefanya ushirikiano wa kubadilishana picha za video na habari na Shirika la Televisheni la Taifa la China na Shirika la Habari la China Xinhua. Amesema wafanyakazi wa shirika hilo pia walipata mafunzo nchini China kutokana na msaada wa mashirika hayo.

    Mkutano wa kamati ya tatu ya Shirikisho la Vyombo vya Habari vya Video vya Afrika umefanyika leo hapa Beijing, na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka vyombo 20 vya habari vya nchi 20 za Afrika pamoja na wajumbe wa China. Washiriki hao wamebadilishana maoni kuhusu kazi za shirikisho hilo, na ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako