• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri wa ulinzi wa Russia

    (GMT+08:00) 2018-10-19 20:49:44

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri wa ulinzi wa Russia Bw. Sergey Shoygu ambaye yupo ziarani nchini China.

    Rais Xi amesema ushirikiano kati ya China na Russia katika sekta mbalimbali umepata mafanikio makubwa, nchi hizo mbili zimeshirikiana na kudumisha uratibu mzuri katika mambo ya kimataifa, na kuwa nguvu ya kuhimiza amani na utulivu duniani. Aidha, rais Xi amesema uhusiano kati ya majeshi ya nchi hizo mbili ni alama muhimu ya uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili, na pia ni nguzo muhimu ya maendeleo ya ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo.

    Bw. Shoygu amesema uongozi wa kimkakati wa rais Vladimr Putin wa Russia na rais Xi wa China ni msingi muhimu wa kukuza zaidi uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili. Amesema Russia inapenda kushirikiana na China kuinua kiwango cha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na uhusiano kati ya majeshi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako