• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wasema China ina uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiuchumi

    (GMT+08:00) 2018-10-22 09:52:22

    Wataalamu wa China wamesema, ingawa China inakabiliwa na changamoto za ndani na nje, lakini inaweza kudumisha maendeleo tulivu ya uchumi kutokana na sera za kuhimiza ongezeko la uchumi.

    Takwimu mpya zinaonesha kuwa katika robo tatu zilizopita mwaka huu, thamani ya pato la ndani la taifa GDP nchini China iliongezeka kwa asilimia 6.7, na thamani hiyo ya robo ya tatu iliongezeka kwa asilimia 6.5, ambayo ilishuka ikilinganishwa na robo ya kwanza na ya pili mwaka huu.

    Ripoti iliyotolewa na kituo cha utafiti wa mambo ya fedha cha Benki ya Mawasiliano ya China imesema, hali hii inatokana na athari ya nje na kushuka kwa kasi ya ongezeko la uwekezaji katika miundombinu.

    Ripoti imesema uwekezaji wa miundombinu unatarajiwa kuongezeka tena kwa haraka baada ya serikali kutekeleza sera chanya kuanzia mwezi Agosti, na China hatimaye inaweza kutimiza lengo lake la kuendeleza uchumi kwa asilimia 6.5 kwa mwaka huu.

    Profesa mshiriki wa Taasisi ya Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Peking Bw. Yan Se amesema, mbali na sera za kuhimiza uwekezaji wa miundombinu na matumizi ya ndani, serikali kuu ya China pia itatumia njia mbalimbali za kifedha kukabiliana na hali ya msukosuko wa kimataifa, ili kudumisha utulivu wa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako