• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • "Safari ya mwaka 2018 ya watu mashuhuri wa nchi za Njia ya Hariri nchini China"--kituo cha mtaa wa Beilin mjini Xi'an

  (GMT+08:00) 2018-10-22 15:51:52

  Tarehe 18, wajumbe kadhaa kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Uturuki, Misri na Palestina, waliohudhuria shughuli ya awamu ya 6 ya "Safari ya mwaka 2018 ya watu mashuhuri wa nchi za Njia ya Hariri nchini China", walitembelea mtaa wa Beilin wa mji wa Xi'an ambao umechanganya utamaduni wa kijadi na mambo ya kisasa.

  Watu mashuhuri kutoka nchi za Njia ya Hariri watembelea mtaa wa Beilin wa mji wa Xi'an.

  Katibu wa mtaa wa Beilin wa mji wa Xi'an Bw. Liu Qizhi anafahamisha mtaa huo

  Naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Barabarani cha Xi'an Bw. Xi Guang anatoa hotuba

  Mkuu wa ofisi ya uenezi ya mtaa wa Beilin Bw. Liu Chunlin anaendesha mkutano

  Bw. Liu Qizhi alipofahamisha hali ya mtaa wa Beilin, alisema mtaa huo unawakaribisha wageni kutoka nchi za Njia ya Hariri, na kupenda kufanya mawasiliano na ushirikiano na nchi hizo kwa kina zaidi.

  Naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Barabarani cha Xi'an Bw. Xi Guang alisema, chuo hicho kilianzisha "Umoja wa Vyuo Vikuu vya Njia za Hariri"mwezi Mei mwaka 2015, ili kuhudumia maendeleo ya jamii na mawasiliano ya kimataifa ya sayansi.

  Matangazo kwa lugha na njia tofauti yasaidia mtaa wa Beilin kujulikana duniani

  Naibu mkurugenzi wa idara ya Asia ya magharibi na Afrika ya Shirika la Utangazaji la China bibi Han Mei anatoa hotuba

   Naibu mkurugenzi wa idara ya Asia ya magharibi na Afrika ya Shirika la Utangazaji la China bibi Han Mei alisema, awamuya 6 ya "Safari ya watu mashuhuri wa nchi za Njia ya Hariri nchini China" iliyoanza kwenye mtaa wa Beilin wa Xi'an, si kama tu ni mazungumzo ya Njia ya Hariri kati ya zama za sasa na kale, bali pia ni hatua halisi ya kuhimiza maelewano ya watu kutokana na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Shughuli hiyo ya watu mashuhuri wa nchi za Njia ya Hariri kutembelea mtaa wa Beilin itaenezwa kupitia tovuti za lugha mbalimbali zikiwemo Kiingereza, Kituruki, Kiarabu na Kiswahili, ChinaNews, na tovuti za mawasiliano ya kijamii ya China na nchi za nje, ili kufahamisha mafanikio ya mtaa huo tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango kwa dunia nzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako