• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu mashuhuri wa nchi za Njia ya Hariri watembelea mtaa wa Beilin wa mji wa Xi'an

  (GMT+08:00) 2018-10-22 16:08:18

  Tarehe 18, watu mashuhuri kadhaa kutoka nchi za Njia ya Hariri zikiwemo Uturuki, Misri na Palestina, walihudhuria awamu ya 6 ya "Safari ya mwaka 2018 ya watu mashuhuri wa nchi za Njia ya Hariri nchini China" pamoja na waandishi wa habari wa China. Pia walitembelea mtaa wa Beilin wa mji wa Xi'an, ambao umechanganya utamaduni wa kijadi na mambo ya kisasa.

  Katibu wa mtaa wa Beilin wa mji wa Xi'an Bw. Liu Qizhi

  Naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Barabara cha Xi'an Bw. Xi Guang

  Mkutano wa kutambulisha mtaa wa Beilin ulifanyika tarehe 18 alasiri katika Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Barabara mjini Xi'an. Katibu wa mtaa wa Beilin wa mji huo Bw. Liu Qizhi, na naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Mawasiliano ya Barabara cha Xi'an Bw. Xi Guang walikutana na ujumbe wa watu mashuhuri wa nchi za Njia ya Hariri ulioongozwa na naibu mkurungezi wa idara ya Asia ya Magharibi na Afrika ya Radio China Kimataifa (Shirika la Utangazaji la China) bibi Han Mei. Pande hizo mbili zilibadilishana maoni kuhusu jinsi mtaa wa Beilin unavyofanya mawasiliano na ushirkiano na nje kutokana na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Bw. Liu Qizhi alisema, mawasiliano na muungano ni sehemu muhimu ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", hivyo shughuli kama "Safari ya watu mashuhuri wa nchi za Njia ya Hariri nchini China" ina umuhimu mkubwa.

  Naibu mkurugenzi wa idara ya Asia ya magharibi na Afrika ya Radio China Kimataifa (CRI) bibi Han Mei

  Bi. Han Mei alisema, shughuli ya watu mashuhuri wa nchi za Njia ya Hariri kutembelea mtaa wa Beilin itaenezwa kupitia tovuti za lugha mbalimbali zikiwemo Kiingereza, Kituruki, Kiarabu na Kiswahili, ChinaNews, na tovuti za mawasiliano ya kijamii za China na nchi za nje, ili kufahamisha mafanikio ya mtaa huo tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango kwa dunia.

  Mhariri mkuu wa kituo cha habari cha tovuti ya CRI Online Shi Jia alisema, tovuti hiyo inafanya ushirikiano na mtaa wa Beilin mara kwa mara, na anatumai shughuli hiyo itasaidia kuhimiza mawasiliano na ushirikiano kati ya mtaa wa Beilin na nchi husika.

  Awamu ya 6 ya "Safari ya watu mashuhuri wa nchi za Njia ya Hariri nchini China" iliyoanza kwenye mtaa wa Beilin wa Xi'an, si kama tu ni mazungumzo ya Njia ya Hariri kati ya zama za sasa na kale, bali pia ni hatua halisi ya kuhimiza maelewano ya watu kutokana na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako