• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Je, nani anaiweka Taiwan Hatarini?

    (GMT+08:00) 2018-10-22 17:13:58

    Makamu wa rais wa Marekani Bw. Mike Pence ametoa hotuba akiilaumu China kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani, kupinga utaratibu wa kimataifa na kutishia utulivu wa mlango bahari wa Taiwan. Aidha, hivi karibuni jeshi la Marekani pia lilianza kuingilia katika suala la Taiwan, vitendo ambavyo vinaweza kuharibu uhusiano kati ya China na Marekani na kati ya China bara na Taiwan. Mbali na hayo hatua ya kujibu vitendo vya Marekani iliyochukuliwa na utawala wa kiongozi wa Taiwan Bibi Cai Yingwen pia itaiweka Taiwan hatarini.

    Marekani inaichokoza China kupitia suala la Taiwan na kuanzisha vita vipya kati ya nchi mbili ili kuhamisha migongano yake ya ndani. Ili kushinda uchaguzi mdogo wa Marekani, serikali ya nchi hiyo inataka kuhamisha wasiwasi wa kisiasa kutokana na shinikizo la hali ya siasa ya ndani. Ikulu ya Marekani imeishutumu mara nyingi China kuwa iliingilia uchaguzi mkuu wa Marekani ili iokoe hali ya uchaguzi mdogo na kuhamisha ufuatiliaji wa umma pamoja na kukwepa wajibu. Kama mtafiti wa idara kuu ya ujasusi ya Marekani Bw. Chris Johnson alivyosema, chama cha Republican kinajaribu kujenga taswira kwamba kura yoyote inayopigiwa na chama cha Democratic inapigiwa kwa ajili ya China.

    Chombo cha habari cha Marekani AXIOS kimesema, serikali ya Marekani inapanga mpango mkubwa wa kupambana na China, ikiwemo kuishambulia China kupitia kisingizio cha kuingilia uchaguzi mkuu. Jarida la Marekani Sera ya Kidiplomasia limesema, Marekani itatenga dola bilioni 700 za kimarekani kuizuia China kutimiza mabadiliko ya kimkakati. Hivi sasa, Sera ya Marekani kwa China imebadilika kutoka hatua za "Kugusa na Kuzuia" hadi hatua za pande zote za kizuizi cha kisiasa, kikwazo cha kanuni, kuzingira kwa njia za kidiplomasia, shinikizo la juu la kiuchumi na maandalizi ya kijeshi.

    Katika miezi mitatu iliyopita, ndege za kivita za China zilisimamisha operesheni za kuizingira Taiwan, hali ya kisiasa ya mlango bahari wa Taiwan imekuwa na utulivu. Wakati Marekani ikianzisha vita vya kibiashara kati yake na China, Marekani kufanya mazoezi makubwa ya kijeshi katika bahari ya kusini, bahari ya Taiwan na bahari ya Pasifiki ni uchokozi na ni majaribu kwa China ili kuilazimisha kujibu vikali na kuongeza nafasi za kufanya mjadala.

    Aidha, Marekani sio mlinzi wa Taiwan. Serikali ya Marekani ya awamu hii imechukua hatua za wazi za kuipendelea Taiwan na kuipinga China. Marekani imeichukulia Taiwan kama kifaa cha kuizuia China. Lakini bila ya kujali jinsi uhusiano kati ya Marekani na Taiwan unavyokua, pande hizo mbili haziwezi kuepusha utaratibu wa "Marekani Kwanza". Kwa mujibu wa kitabu kipya cha "Hofu: Trump katika Ikulu ya Marekani" kilichotolewa hivi karibuni, rais Donald Trump wa Marekani aliyekuwa mfanyabiashara hana mapenzi yoyote na Taiwan, na hafahamu sana uhusiano huo. Anachofuatilia zaidi ni kuwa Marekani itapata nini kutokana na kuilinda Taiwan. Tangu rais Trump aingie madarakani, amepitisha miswada miwili ya kuiuzia Taiwan silaha na kujaribu kuhimiza mauzo ya silaha kwa Marekani kuwa jambo la kawaida na muungano wa viwanda vya utengenezaji wa silaha. Wafanyabiashara wa Marekani pia wanataka kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande mbili na kuihimiza Taiwan kufungua soko lake la nyama za nguruwe na ng'ombe kwa Marekani. Lakini ukweli ni kwamba Marekani inaitoza Taiwan ada za ulinzi.

    Sera ya serikali ya Trump kwa Taiwan ni kuitaka Taiwan kutoa faida na msaada kwa maslahi ya kimkakati ya Marekani. Kama rais Trump akifikia makubaliano na China bara, maslahi ya Taiwan yanaweza kutupwa wakati wowote. Hivyo, nguvu ya kuitenganisha Taiwan na China ni chanzo cha kuiweka Taiwan hatarini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako