• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Uchuuzi wa samaki barabarani wapigwa marufuku

    (GMT+08:00) 2018-10-22 20:18:29

    Ole wako mchuuzi wa samaki katika barabara ya Nakuru kuelekea Nairobi.

    Onyo hili limetolewa na idara ya afya iliyopiga marufuku uchuuzi wa samaki barabarani kwa misingi ya afya na mkurupuko wa maradhi.

    Mkurugenzi wa idara ya afya katika kaunti ya Nakuru Samuel King"ori ameonya kwamba mfanyibiashara yeyote atakaekiuka agizo hilo atatiwa mbaroni na kushtakiwa.

    Licha ya kwamba biashara hiyo imetoa ajira kwa zaidi ya mamia ya vijana na wanawake ,wanunuzi wamelalamikia ukosefu wa usafi katika mapishi na hata mauzo ya samaki hao.

    Kaunti ya Nakuru sasa imepanga kuanzisha vituo vya kisasa vya kuuza samaki na pia kuwahifadhi katika mazingira safi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako