• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SGR, Reli yangu
  Hadithi ya Patrick na Rapahel, wajenzi wa SGR

  (GMT+08:00) 2018-10-23 10:10:57

  Kwenye makala yetu ya hadithi za SGR leo mwandishi wetu ametuandalia ripoti kuhusu na Kennedy Mugo na Chelangat Sharon, wahudumu wa wa abiria kwenye treni mpya ya SGR kati ya Nairobi na Mombasa.

  Ndio nguvu kazi ya ujenzi wa reli ya kisasa SGR nchini Kenya.

  Vijana kwa wazee.

  Kampuni inayotekeleza mradi huu wa reli imekuwa nchini Kenya kwa zaidi ya miaka 20 ikitekeleza mirafi mingine kama vile barabara.

  Lakini kwa wakenya wengi wanaofanya kazi hapa mradi wa reli umewaletea sio tu ajira lakini pia na uzoefu wa kipekee.

  Ndio reli ya kwanza ya aina yake katika kanda ya Afrika Mashariki.

  Teknolojia ni ya hali ya juu, na hivyo wafanyakazi wanapokea mafunzo kutoka kwa wataalama wa China ili kuendelea na ujenzi.

  Patrick Nthiga amefanya kazi na CRBC kuanzia mwaka 2008 na sasa anahusika na ujenzi wa awamu ya pili ya reli kati ya Nairobi na Narok.

  Siku chanche baada ya kujiunga na mradi wa reli alipandihwa cheo na kuwa msimamizi wa kazi za uashi.

  "Ili niwe msimamizi kuanzia Mtito mpaka sasa nimefanya kazi ya ubora wa juu. Hii ndio taaluuma yangu, ya kujenga. Licha ya changamoto nyinhgi kama vile kukutana na wachina ambao hawaelewi lugha, lakini unajikakamua mpaka unaelewa vile wanaongea."

  Kwa kufanya kazi hapa kwenye SGR maisha ya familia yake yameendelea kuimarika siku hadi siku.

  Amefanikiwa kujenga nyumba na kusomesha watoto wake na sasa anaona hata baada ya kustaafu, familia yake imara.

  "Niko na msichana ambaye anaitwa Dkt Jemimah Mwendia Nthiga ambaye sasa anafanya kazi katika hospitali ya Kieni. Hivyo kwangu naona kazi hii ina faida. Pia niko na mifugo kwa boma yangu na nimejenga nyumba zuri na labda baada ya miaka miwili au mitatu napanga kununua gari"

  Hadithi ya Patrick ni sawa na ya kijana Joseph Kimotho ambaye maisha yake yambadilika kutokana na ajira kwenye mradi wa SGR.

  "Nilikuwa nafanya kazi huko rongai na sasa niko hapa kwa karibu mwaka mmoja, kazi hi imenisaidia kwa sababu familia yangu inaishi vizuri na nimewawekea biashara na niko sawa. Hata saa nikipelekwa kuendelea kujenga mbele niko na ujuzi wa kujenga reli na sikuwa najua"

  Hadi sasa zaidi ya wakenya 30,000 wanafanya kazi kwenye mradi huu ambao ndio ni mkubwa zaidi kwa utoaji wa ajira nchini Kenya.

  Na mbali na kufanya kazi pia wanaendelea kupata mafunzo ya kiufundi ambayo yatawasaidia kufanya ukarabati wa reli baada ya wawekezaji wa China kuondoka.

  Mzee Rapahel Syengo ni mmoja wa wale waliofanya kazi kwa muda mrefu hapa.

  "Uzoefu wangu kwenye hii kazi naona umeimarika sana. Kuna vitu abayo nilikuwa najua, lakini kuna mambo mengine nimejifunza hapa kwa mfano kuelekeza maji kwenye mitaro ili kuepusha mmomonyoko wa udongo, hiyo sikuwa najua lakini sasa nimejua"

  Syengo anaona kwamba manufaa ya kufanya kazi kwenye mradi huu sio tu ya moja kwa moja kwa mtu aliyeajiriwa lakini pia na kwa jamii yote.

  "Kufanya kazi kujenga reli ina manufaa mengi kwa sababu wale watu wanafanya kazi hapa wanasaidia familia nyingi, na kuna wengine wana watoto shuleni wanawalipia karo na wengine wanasaidia jamaa zao kuwapeleka hospitali, kwa hivyo unaona kwamba wananufaika. Kwa upande wangu naweza kusema ina manufaa sana "

  Wakenya wengi hapa wanafurahia muundo mpya wa reli ya SGR ikilinganishwa na reli ya zamani iliojengwa miaka mia moja iliopita.

  Kwa mfano kwenye hifadhi za wanyama pori kuna daraja za kuwezesha wanyama kutembea huru na ua wa kuzuia mifugo au watu kuigia kwenye eneo hatai ya njia ya reli.

  Kutokana na bidii yake kazini, Patrick Nthiga amepata uaminifu mkubwa kutoka kwa waajiri wake.

  Bali na kumpa jukumu la kusimamia kazi, pia wanaweka imani kubwa kwake kwamba atafanikisha kwa ubora unaotakiwa.

  "Ni lazima kwanza bosi wangu aniambie kuwa leo tutafanya kazi hi na hii na kuanzia hapo sasa nachukua usukani kwa sababu bosi wangu hawezi kupanga watu na baadaye wakimaliza kazi wananiita ili nihakikishe kwamba kila kitu kiko sawa "

  Mzee Rapahel Syengo pia anaona kuwa ushirikiano mzuri kati ya wachina na wakenya umerahisisha kazi, na sasa wenyeji wanafanya kazi bila kusimamiwa.

  "Kwa mfano sehemu kama ile kuna mchina mmoja tu na yuko na wakenya zaii ya 50, kwa hivyo akija asubuhi anapeana tu karatasi na jioni anarudi kuangalia kama kazi imefanyika vizuri, watu wamezoea kazi"

  Mpango wa baadaye ni kwamba wakenya wenyewe watasimamia na kuendesha reli hii ya kisasa bila msaada wa wataalam wa China.

  Lakini kabla ya hapo tayari serikali za pande zote mbili zimeendelea kutoa mafunzo katika kila ngazi, kuanzia ujenzi, uendeshaji, ukarabati na ufundi ili kuhamisha kikamilifu utaalam wa oparesheni za reli kutoka China hadi Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako