• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Paul Biya achaguliwa tena kuwa rais wa Cameroon

    (GMT+08:00) 2018-10-23 09:57:47

    Matokeo yaliyotolewa jana na kamati ya katiba ya Cameroon yameonyesha kuwa mgombea urais kutoka chama tawala cha RDPC ambaye ni rais wa sasa wa Cameroon Paul Biya ameshinda kiti cha urais kwa muhula wa saba kwa kupata asilimia 71.28 ya kura, ikifuatwa na mpinzani wake Bw Maurice Kamto kutoka chama cha upinzani cha Movement for the Rebirth of Cameroon (MRC) aliyepata asilimia 14.23 ya kura.

    Takwimu zinaonesha kuwa kwenye uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 7 mwezi huu, watu takriban milioni 3.59 walijitokeza kwenda kupiga kura, idadi ambacho ni asilimia 53.85 ya wapiga kura walioandikishwa, lakini kwenye maeneo yanayotumia lugha ya Kiingereza, ni chini ya asilimia 10 tu ya watu walipiga kura zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako