• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao lazinduliwa rasmi

    (GMT+08:00) 2018-10-23 19:12:41

    Rais Xi Jinping wa China leo huko Zhuhai, kusini mwa China ametangaza uzinduzi rasmi wa daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao. Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 55 lililosanifiwa na kujengwa kwa miaka 15 limeanza kutoa huduma.

    Daraja la Hong Kong- Zhuhai-Macao ni mradi mrefu na mgumu zaidi wa kuvuka bahari duniani ambao pia ni mradi unaojengwa kwa mara ya kwanza na mkoa wa Guangdong, Macao na Hong Kong. Daraja hilo limetimiza kwa mara ya kwanza muungano wa barabara kati ya Zhuhai, Macao na Hong Kong, huku likipunguza muda wa usafiri kutoka Hong Kong hadi Zhuhai na Macao kutoka saa 3 hadi dakika 45. Mbunifu mkuu wa daraja hilo Bw. Meng Fanchao amesema, daraja hilo litabadilisha utaratibu wa jamii, uchumi na mawasiliano katika eneo la Dawan, kuwawezesha watu kufungua ukurasa mpya wa mtindo wa maisha na kuleta faida ya dola bilioni zaidi ya kumi za kimarekani.

    Maisha mazuri yanatokana na uvumbuzi. Katika ujenzi wa daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao, vifaa vipya, ufundi mpya, mashine mpya na teknolojia mpya zimetumiwa sana, na idadi ya hataza imefikia zaidi ya 400. Mhandisi mkuu wa idara ya usimamizi ya daraja hilo Bw. Su Quanke amesema, daraja hilo ni la teknolojia na uvumbuzi. Nyuma ya changamoto hizo za ngazi ya dunia, nguvu ya uvumbuzi na sayansi na teknolojia zinaunga mkono daraja hilo.

    Ili kukabiliana na changamoto za usimamizi wa ujenzi, teknolojia za mradi, hifadhi ya mazingira na usalama wa bahari, ujenzi wa daraja hilo umetumia wazo la utengenezaji wa viwanda, ambalo linaweza kukinga kimbunga cha ngazi ya 16, tetemeko la ardhi lenye ngazi ya 7 kwenye kipimo cha Richter, na muda wake wa matumizi unaweza kudumu miaka 120.

    Moja ya malengo ya ujenzi wa eneo la Dawan la Guangdong-Hong Kong-Macao ni kuwa kituo kipya cha dunia cha sayansi na teknoloji. Ni imani kuwa kufuatia uzinduzi wa daraja hilo, uvumbuzi wa eneo la Dawan utaendelezwa zaidi na kuongoza maendeleo ya uchumi wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako