• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kagame alitaka bunge la Afrika kufanikisha soko huru Afrika

    (GMT+08:00) 2018-10-23 19:52:42

    Rais wa Rwanda Paul Kagame amelitaka bunge la Afrika kusaidia kuidhinishwa kwa haraka kwa soko huru la bara hilo hasa usafirishaji huru wa bidhaa na watu.

    Kagame ambaye ni mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika amesema kuanza kutekelezwa kwa soko hilo kutasaidia Afrika kufikia lengo lake la agenda ya mwaka 2063.

    Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha wiki mbili cha bunge hilo.

    Makubaliano ya biashara huru na soko la pamoja la Afrika yalisainiwa mjini Kigali Machi 21 mwaka huu na tayari nchi 44 zimekubali kujiunga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako