• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Maafisa wa AfDB wazuru Mbeya

    (GMT+08:00) 2018-10-23 20:13:21

    Kundi la wataalam kutoka benki ya maendeleo ya Afrika AfDB liko eneo la mbeya nchini Tanzania kutafiti maeneo muhimu ya kuwekeza viwanda vya bidhaa za kilimo.

    Kundi hilo linajiunga na maafisa kutoka kwa wizara ya biashara na limetembelea shamba la viazi kwa jina STAWISHA kama sehemu ya utafiti wake.

    Akizungumza baada ya kukutana na wataalam hao, kamishena wa Mbeya Albert Chalamila amesema AfDB itawekeza kwenye miradi ya kuongeza thamani ili kusaidia wakulima na hasa vijana kuongeza mapato yao.

    Alisema ziara ya maafisa hao inafutatia makubaliano ya rais John Magufuli na mkuu wa AfDB Akinwumi Adesina

    Bidhaa za kilimo zitakazopewa kipaumbele ni pamoja na mahindi,alizeti, maparachichi maziwa na kahawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako