• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani kujitoa katika mkataba wa silaha za masafa ya kati za nyuklia kutaharibu msingi wa amani wa dunia

  (GMT+08:00) 2018-10-24 19:03:05

  Rais Vladimir Putin wa Russia amekutana na msaidizi wa rais wa Marekani anayeshughulikia mambo ya usalama wa taifa Bw. John Bolton ambaye yuko ziarani nchini Russia. Mkutano huo umefanyika chini ya uamuzi wa rais Donald Trump wa Marekani kutangaza kujitoa katika Mkataba wa Silaha za Masafa ya Kati za Nyuklia. Rais Putin amekosoa madai ya Marekani kuhusu Russia kutofuata mkataba huo, na Bw. Bolton amejibu kuwa hajakwenda Russia kwa nia ya kumaliza suala hilo. Pande zote mbili hazijapata makubaliano yoyote juu ya mkataba huo ndani ya mkutano wa dakika 90.

  Mkataba wa silaha za masafa ya kati za nyuklia ulisainiwa Desemba 8 mwaka 1987 kati ya Jamhuri ya Kisovieti na Marekani. Mkataba huo umesema, nchi hizo mbili haziwezi kuhifadhi, kutengeneza au kufanya jaribio la makombora yenye masafa ya kilomita 500 hadi 5500. Mkataba huo ulitekelezwa kwa pande zote mwezi wa Mei mwaka 1991, ambapo Jamhuri ya Kisovieti iliteketeza makombora 1752 na Marekani iliteketeza makombora 859. Lakini kila upande unaweza kusimamisha mkataba huo kutokana na kutoa ushahidi. Ziara ya Bw. Bolton nchini Russia inalenga kuithibitishia Russia kuwa Marekani inataka kujitoa katika mkataba huo.

  Swali ni je, kwa nini Marekani inataka kujitoa kutoka mkataba huo? Ni dhihiri kwamba hatua hiyo inalenga kutimiza mkakati wa "Marekani Kwanza".

  Marekani inataka kuimarisha tena jeshi lake na maendeleo ya silaha. Wakati wa kampeni zake za urais, Trump alisema kuwa kama akiingia madarakani, ataendeleza kwa nguvu jeshi la Marekani, ukiwemo ufundi husika wa makombora ya ngazi ya juu. Muswada wa mwaka wa bajeti ya ulinzi wa taifa mwaka 2018 umeitaka wizara ya ulinzi wa taifa kuendeleza na kutafiti mfumo wa makombora ya masafa ya kati. Ili kutimiza lengo hilo, Marekani inatakiwa kuvunja mkataba huo. Mbali na hayo, kwa ajili ya kuzidi kuimarisha viwanda vya utengenezaji wa silaha vya Marekani, serikali ya nchi hiyo inataka kuondoa vizuizi vya mkataba huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako