• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakazi wa Nairobi kutozwa ushuru maradufu

    (GMT+08:00) 2018-10-24 20:47:13

    Huenda wakazi wa Nairobi,nchini Kenya,huenda wakalazimika kulipa ushuru zaidi kutokana na mapendekezo ya mswada wa fedha.

    Mswada huo wa fedha umependekeza kuanzishwa kwa aina mpya za madaraja ya ushuru wa ziada katika baadhi ya sekta,kwa lengo la kujazilia nakisi ya bajeti ya 2018/2019.

    Mswada huo unapendekeza kuwa na ushuru mpya katika uokotaji wa takataka mitaani ambapo wanaoishi katika mitaa ya mabanda watalipa Sh100 kila mwezi.

    Aidha watu wanaoishi mitaa ya wastani watalipa Sh300 kwa mwezi ilhali wanaoishi katika mitaa ya kifahari watalipa Sh500 kwa mwezi.

    Shule pia hazijasazwa katika ada hii mpya ambapo ambapo shule za kutwa, chekechea na zilizo na wanafunzi zaidi ya 850 zitatakiwa kulipa Sh30,000 kwa mwezi mmoja.

    Shule za msingi za mabweni, sekondari, vyuo viku na taasisi za mafunzo ya juu zilizo na wanafunzi zaidi ya 2,000 zitalipa kufikia Sh65,000.

    Kuegesha magari ya kibinafsi kutagharimu Sh400 kutoka Sh300 kwa siku.

    Huenda mashine zote za ATM jijini zikatozwa ushuru, mabango ya matangazo yataongezewa ushuru pamoja na michezo ya kujipumbaza na bahati nasibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako