• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SGR, Reli yangu
  Hadithi ya Sera, abiria wa SGR

  (GMT+08:00) 2018-10-25 09:31:06

  Kwenye makala yetu ya hadithi za SGR leo mwandishi wetu anazungumza na abiria wanaofurahia huduma za usafiri kwenye treni mpya ya SGR.

  Ni safari ya kwenda Mombasa kwa kutumia treni mpya ya SGR.

  Umbali wa kilomita 472 kati ya mji mkuu Nairobi na mji wa pwani Mombasa.

  Safari ya barabara ni ghali na inachukua masaa 10 hivi lakini kwenye treni ni masaa 4 na nusu tu.

  Baada ya kuwasili nakutana na baadhi ya wasafiri wengi wakiwa ni watalii wa ndani.

  "Nimesafiri na mtoto wangu ana umri wa miezi 9. Nimempandisha treni kwa sababu nina uhakika nayo na nina imani nayo. Safari imekuwa zuri tumefurahia kuona mazingira na pia maendeleo. "

  "Mimi ni mwalimu nafunza katika shule moja ilioko Kajiado. Tumetumia hii SGR ambayo ni ya kisasa na tumefurahi sana kwa sababu sio kama usafiri wa basi. Inafika haraka na ina starehe. Njiani tumeona wanyama na misitu. Tumekuja na wanafunzi 27 na tumekuja ziara ya kimasomo. Nauli yake pia sio kubwa tumelipa dola 7.3 kutoka Emali hadi Mombasa."

  Lakini kati ya abiria hakuna mwenye hadithi ya kipekee kama Sera Wamuyu Kigo.

  "Mara ya kwanza nilipigiwa simu nikaambiwa tuko na zawadi yako, wakati nilienda kwa kituo cha reli nikapewa vocha na nikaambiwa nimezawadiwa kwa sababu ya SGR, lakini sikuambiwa mimi ni abiria nambari miolioni moja. Nilifiriki wanapea kila mtu, na nikafikiri haina umaalum. Lakini baadaye niligundua ni mimi tu nilikuwa nimepewa na ilikuwa ni jambo la kufurahia sana "

  Yeye alikuwa ni abiria nambari milioni moja tangu kuanza kwa oparesheni za SGR juni 2017.

  Alikuwa amesafiri kwenda mjini Voi kutafuta ajira, ingawa hakuipata lakini kusafiria SGR kulimletea yeye na familia yake zawadi ambayo hawakuitarajia.

  "Vocha ilimaanisha kwamba nitasafiri bila kulipa nauli na pia nikapewa hoteli ya English Point Marina kwa siku mbili bila malipo na kula vyakula vyote bila malipo. Ilikuwa ni zawadi kubwa sana kwa sababu ile ni hoteli ya nyota tano, na kulingana na uwezo wangu zingeweza kwenda kwa hoteli kama hiyo.Nilifurahiwa sana."

  Tangu siku ile Sera anasema hatawahi tena kutumia usafiri wa aina nyingine kati ya Mombasa na Nairobi.

  "SGR ni ya muhimu sana na imekuja kusaidia. Zamani ilikuwa ni lazima kutumia ndege au basi.Ukitumia basi inachukua muda mrefu nayo ndege ni pesa nyingi sana kwa mwananchi wa kawaida. Kwenye SGR hakuna msongamano , hakuna wachuuzi, haina kelele wala joto "

  Mara nyingi treni ya SGR inajaa kwa asilimia 99 na huenda ukakosa tiketi iwapo hautanunua siku 10 kabla ya kusaifiri.

  Hii ni ishara kwamba mahitaji ya aina hiyo ya usaifiri bado yanaongezeka na kila mkenya angependa kuhisi mwendo kasi wa kilomita 120 hivi kwa saa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako