• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China aendelea kufanya ukaguzi mkoani Guangdong

    (GMT+08:00) 2018-10-25 16:16:57

    Tarehe 24 rais Xi Jinping wa China alifanya ukaguzi katika miji ya Shenzhen na Guangzhou. Mjini Shenzhen alipotembelea Maonesho ya kuadhimisha miaka 40 tangu mkoa wa Guangdong uanze kufanya mageuzi na kufungua mlango, rais Xi amesema, nia ya ziara yake mjini Shenzhen na mkoani Guangdong kwa mara nyingine, ni kuiambia dunia kuwa China itaendelea na mageuzi na kufungua mlango bila kusita.

    Maonesho ya kuadhimisha miaka 40 tangu mkoa wa Guangdong uanze kufanya mageuzi na kufungua mlango, yanaonesha historia ya miaka 40 ya mkoa wa Guangdong katika kufanya mageuzi na kufungua mlango, kwa kupitia picha za zamani na za sasa. Rais Xi Jinping anasema,

    "Huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kufanya mageuzi na kufungua mlango. katika miaka 40 iliyopita, China imepata mafanikio makubwa, hivyo tutashikilia njia hiyo, hata kama yakiwepo matatizo na masuala kadhaa, tutapiga hatua na kuyatatua njiani. Tutaendelea kushikilia mageuzi na kufungua mlango, wakati huo huo tutainua kiwango chetu bila kusita."

    Tarehe 24 alasiri rais Xi Jinping aliwasili Chuo Kikuu cha Jinan. Alipofanya mazungumzo na wanafunzi vijana aliwataka wajifunze vizuri na kutoa mchango kwa jamii baadaye. Anasema,

    "Kueneza utamaduni wa jadi wa China kwenye nchi mbalimbali, huu ni moyo wa Chuo Kikuu cha Jinan, tutaeneza moyo huu. Mimi naona wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali, baada ya kuhitimu kwenye chuo cha hapa, nina matumaini nyinyi mtakuwa watu wenye ujuzi na mtaweza kutafuta hadhi yenu kwenye jamii. "

    Kituo cha mwisho cha ukaguzi katika siku hiyo kilikuwa kampuni ya zana za magari ya Mingluo mjini Guangzhou. Rais Xi Jinping alifanya mazungumzo na wakurugenzi wa kampuni binafsi ndogo na za ukubwa wa kati. Rais Xi aliwasifu kwa mafanikio ya uvumbuzi. Anasema,

    "Kampuni ndogo na za ukubwa wa kati zinaweza kupata mafanikio makubwa. Kamati kuu ya Chama inatilia maanani sana kampuni hizo pia inafanya juhudi za kuhimiza maendeleo ya kampuni hizo. Hii itaufanya uchumi wa nchi yetu uendelezwe kwa pande zote, kwa njia ya kisayansi, na kwa sifa za juu. Tunatetea kuanzisha shughuli na kufanya uvumbuzi, hii imetoa fursa nyingi zaidi kwa kampuni ndogo na za ukubwa wa kati, pia hatuwezi kuacha kampuni hizo. Nawataka wamiliki wote wa kampuni ndogo na za ukubwa wa kati kufuatilia shughuli zao kuu, kuimarisha uvumbuzi, na kufanya jitihada ili kuleta faida zaidi kwa kampuni zao na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa taifa letu na wananchi wetu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako