• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kipengele cha 301 chaonesha jaribio la Marekani la kuzuia maendeleo halali ya China

  (GMT+08:00) 2018-10-25 17:31:34

  Hivi karibuni Kituo cha Kusini kilichoundwa na nchi 50 zinazoendelea kimetoa ripoti inayoitwa "Kipengele cha 301 cha Marekani: Kwa nini ni haramu na kinapotosha?". Ripoti hiyo imevutia tena ufuatiliaji wa jumuiya ya kimataifa katika kipengele hicho chenye utata.

  Kituo cha Kusini kilizinduliwa mwaka 1995, na kinafanya juhudi kuzidisha mshikamano na ushirikiano kati ya kusini na kusini na kuimarisha maelewano na ushirikiano kati ya Kusini na Kaskazini juu ya msingi wa usawa na haki. Ripoti hiyo mpya iliyotolewa na kituo hicho imeeleza historia ya kipengele cha 301 cha Marekani na lawama kwa China pamoja na vitendo haramu vya kupotosha vya Marekani.

  Chimbuko la kipengele cha 301 ni sheria ya biashara ya mwaka 1974 ya Marekani, ambavyo ni kifaa muhimu cha wafanyabiashara wa Marekani kupanua soko la nje. Kwa mfano, mwaka 1975, wafanyabishara wa mayai wa Marekani walitumia kipengele hicho kuitaka serikali ya nchi hiyo kuchunguza hatua ya Canada kuweka kiwango cha uagizaji ili kufungua soko la nje. Katika miaka ya 80 na 90 karne iliyopita, kipengele hicho kinajulikana zaidi kutokana na sifa mbaya katika biashara ya kimataifa. Marekani ilitumia kipengele hicho mara nyingi kufanya uchunguzi kwa vitendo vya biashara vya nchi mbalimbali ikiwemo Japani.

  Mwaka 1995, Shirika la Biashara Duniani WTO lilizinduliwa, ambalo lilipandisha kiwango cha makubaliano makuu ya ushuru na biashara na kuweka mfumo wa kutatua migongano ya kibiashara. Mtaalamu wa masuala ya biashara wa taasisi ya uchumi wa kimataifa ya Peterson Bw. Chad Bown amesema, mfumo wa kutatua migongano ya kibiashara wa WTO umeepusha kitendo cha kihuni cha kutumia kipengele cha 301 cha Marekani.

  Ripoti ya Kituo cha Kusini imesema, hatua ya Marekani kutumia tena kipengele cha 301 inashtua WTO. Lawama ya uchunguzi wa 301 wa Marekani dhidi ya China inatumia kigezo cha Marekani na sio kigezo cha WTO. Kwa mfano, ukabidhi wa teknolojia, kampuni za ubia za pamoja na mchakato wa kutoa idhini katika soko la China zote ni hatua zilizofanywa na kampuni kutokana na mkataba. Ripoti inaona kuwa, kampuni za Marekani zinazowekeza China zinasaini mkataba kwa hiari, kwa sababu kampuni hizo zinafahamu zitapata faida kubwa katika soko hilo. Lakini serikali ya Marekani imeilaumu China kwa kuunga mkono maendeleo ya viwanda na teknolojia na kuharibu hakimiliki ya ujuzi.

  Ripoti hiyo pia imeorodhesha maendeleo makubwa ya ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi yaliyopatikana nchini China, huku ikisema uvumbuzi wa teknolojia unatokana na ongezeko la uwekezaji wa China katika utafiti. Kwa mfano, hivi sasa thamani ya uwekezaji wa China katika utafiti imechukua asilimia 20.8 ya thamani ya ujumla ya dunia, ambayo ni sawa na ujumla wa uwekezaji wa nchi zote za Ulaya katika sekta hiyo.

  Mwanauchumi Bw. John Mcmillan ameeleza kuwa mfumo wa pande nyingi ni kuwa "kama ukinisaidia, nitakusaidia vilevile", lakini ukweli wa kipengele cha 301 ni kwamba "angalau utanisaidia, ama sivyo nitakuharibu".

  Ripot hiyo inakamilisha kwa kusema kuwa, chanzo halisi cha serikali ya Marekani kutumia kipengele cha 301 hakihusiani na biashara, kinyume chake ni kuwa Marekani inajaribu kuizuia China kuhimiza maendeleo ya viwanda na teknolojia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako