• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Marufuku kuuza kahawa ghafi,yasema TACRI

    (GMT+08:00) 2018-10-25 20:02:57

    Taasisi ya utafiti wa kahawa nchini Tanzania (TACRI) imepiga marufuku wakulima kuuza kahawa ghafi kwa kuwa zinashusha thamani na ubora wa zao hilo.

    Utafiti unaonyesha kuuza kahawa ya maganda,ambayo haijachakachwa ,kunapunguza ubora wa zao hilo na hivyo kushusha thamani katika soko la dunia.

    Akizungumza katika ziara ya maofisa wa kijeshi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika,mkoani Arusha jana,Mkurugenzi Mtendaji wa TACRI,Dk Deusdedit Kilambo,alisema kwa sasa zao la kahawa halitaruhusiwa kuuzwa likiwa na maganda yake.

    Aliongeza kuwa itakuwa ni jambo la aibu kama serikali ikiendelea kuwaacha watu kuuza zao hilo bila kukobolewa kitaalamu kwani kwa kufanya hivyo ni kuipunguza thamani na ubora na bei hushuka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako