• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wakuu wa China na Japan wahudhuria tafrija ya maadhimisho ya miaka 40 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa amani na urafiki kati ya China na Japan

    (GMT+08:00) 2018-10-26 09:41:30

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana mchana pamoja na mwenzake wa Japan Bw. Shinzo Abe ambaye yupo ziarani nchini China, wamehudhuria na kuhutubia tafrija ya maadhimisho ya Miaka 40 tangu kusainiwa kwa Makubaliano ya amani na urafiki kati ya China na Japan yaliyofanyika katika Jumba la Mikutano ya Umma hapa Beijing.

    Bw. Li Keqiang amesema China inaendeleza mageuzi kwa pande zote, kuharakisha mchakato wa kubadilisha msukumo wa maendeleo, ili kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu. Amesema China inakaribisha Japan kushiriki kwenye mchakato huo wa China, na kufungua kwa pamoja ukurasa mpya wa ushirikiano wa kunufaishana.

    Kwa upande wake Bw. Shinzo Abe amesema makubaliano ya amani na urafiki kati ya China na Japan yameweka kanuni muhimu kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Anatumai kuwa pande hizo mbili zitafanya juhudi kwa pamoja katika kusukuma mbele ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili, ili kutoa mchango kwa ajili ya amani na ustawi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako