• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasukuma mbele sera ya mageuzi na ufunguaji mlango

    (GMT+08:00) 2018-10-26 09:56:54

    Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alipokagua mkoa wa Guangdong alisema, China inapaswa kuendelea kusukuma mbele sera ya mageuzi na ufunguaji mlango kwa pande zote, ili kufanya "mwujiza mkubwa zaidi wa kupongezwa na dunia".

    Hivi leo dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa zaidi katika miaka 100 iliyopita. Hali ya kuwepo kwa ncha nyingi na utandawazi duniani zinaharakisha marekebisho ya utaratibu wa kimataifa na muundo wa uchumi wa dunia, nchi mbalimbali zinahimiza mageuzi na uvumbuzi ili kupata nafasi mpya ya maendeleo, na China pia inaboresha njia ya kuendeleza jamii na uchumi. Wakati huo huo, vitendo vya upande mmoja na kujilinda kibiashara, mfumo wa siasa inayosisitiza uongozi wa umma Populism, pamoja na mikwaruzano ya kibiashara vinaongezeka, na kuleta changamoto kubwa kwa dunia nzima, na pia kuleta athari kwa maendeleo ya uchumi wa China.

    Je, katika hali hizi za kutatanisha duniani, China inapaswa kufanya nini ili kusukuma mbele sera ya mageuzi na ufunguaji mlango? Kwanza, China itaharakisha ujenzi wa uwezo wa uvumbuzi. Kutokana na mpango uliowekwa na mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, hadi kufikia mwaka 2035, China itakuwa moja kati ya nchi zenye uwezo mkubwa zaidi wa uvumbuzi duniani.

    Pili, China itaharakisha kuinua kiwango cha teknolojia za digitali, mtandao wa Internet na akili bandia katika sekta za uzalishaji. Ingawa sekta hizo zimeendelea kwa kasi katika miaka 40 iliyopita, lakini China bado iko sehemu ya chini na ya kati katika mnyororo wa sekta hizo duniani. Rais Xi alipofanya ziara ya ukaguzi mkoani Guangdong, alisisitiza umuhimu wa teknolojia za digitali, mtandao wa Internet na akili bandia, na kudhihirisha kipaumbele cha maendeleo ya sekta za uzalishaji.

    Tatu, China itaanzisha maeneo mapya ya kielelezo cha sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China, China imejenga maeneo 12 ya biashara huria. Mbali na hayo, China inajenga eneo la nne la uchumi la ghuba katika sehemu za Guangdong, Hongkong na Macao, baada ya maeneo mawili ya ghuba ya New York na San Francisco nchini Marekani na eneo la ghuba la Tokyo nchini Japan.

    Nne, China itazingatia zaidi uwiano na uratibu wakati inapojiendeleza. Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulisema, hivi leo shida kubwa zaidi inayoikabili jamii ya China ni pengo kati ya ongezeko la mahitaji ya maisha bora ya wananchi, na hali ya ukosefu wa maendeleo ya kutosha na yenye uwiano. Alipokuwa mkoani Guangdong, rais Xi alitembelea mji ulioendelea zaidi wa Guangzhou, na pia alitembelea sehemu ya Qingyuan yenye watu wengi maskini, ambapo aliagiza kuharakisha maendeleo ya vijiji, na kuhimiza maendeleo yenye uwiano na uratibu.

    Wakati China inaadhimisha miaka 40 tangu ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, ziara ya ukaguzi ya rais Xi mkoani Guangdong inaonesha kuwa, katika dunia hii yenye mabadiliko makubwa, China imetoa jibu lisilobadilika, yaani kuendelea kusukuma mbele sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, na kufanya "mwujiza mkubwa zaidi wa kupongezwa na dunia".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako