• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu za soka eneo la maziwa makuu zaimarika viwango vya FIFA

    (GMT+08:00) 2018-10-26 13:00:49

    Timu za eneo la maziwa makuu Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi zimeimarika katika viwango bora vya soka duniani vilivyotolewa na shirikisho la soka duniani FIFA jana Alhamisi.

    Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepanda nafasi nne zaidi hadi kufikia nafasi ya 136 kutoka nafasi ya 140 mwezi uliopita.

    Harambee stars ya Kenya imechupa kutoka nafasi ya 107 hadi 105, na Uganda imekamata nafasi ya 79 huku Burundi imepanda nafasi sita hadi nafasi ya 142 duniani.

    Ubelgiji imefanikiwa kuiondoa Ufaransa katika nafasi ya kwanza ya viwango vya soka vya dunia vya FIFA, huku Tunisia inaongoza Bara Afrika katika nafasi ya 22 duniani Imeruka juu nafasi moja, Inafuatiwa na Senegal ambayo imeng'ang'ania nafasi ya 25 duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako