• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Al Ahly kumenyana na Esperance de Tunis fainali ya klabu bingwa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-10-26 13:02:03

    Al Ahly ya Misri, itacheza na Esperance de Tunis, ya Tunisia, katika fainali ya kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, itakayofanyika mwezi Novemba.

    Licha ya kufungwa mabao 2-1 na Entente Setif ya Algeria siku ya Jumanne usiku, ilifuzu kwa jumla ya mabao 3-2 kwa sababu ya ushindi wa nyumbani wa mabao 2-0 zaidi ya wiki tatu zilizopita.

    Mabingwa hao mara nane wa taji hili, wataanza kuwa wenyeji wa mchuano wa fainali Novemba 2 jijini Cairo, kabla ya mechi ya mwisho kuchezwa mjini Rades, Novemba 9.

    Esperance de Tunis, nayo ilifuzu baada ya kupata ushindi wa mbao 3-4. Licha ya kufungwa ngenini na Primero de Agostio bao 1-0, ikicheza nyumbani ilifanikiwa kupata ushindi wa manao 4-2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako