• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya Kenya yalenga soko la China

    (GMT+08:00) 2018-10-26 16:39:32

    Maonesho ya kwanza ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China CIIE yatafanyika huko Shanghai. Makampuni ya nchi mbalimbali ikiwemo Kenya yanataka kutumia fursa hiyo kupata faida katika soko kubwa la China. Kenya ni nchi yenye raslimali nyingi ikiwemo kahawa, chai na chakula, na makampuni ya nchi hiyo yanataka kuwawezesha wachina wengi zaidi kuonja utamu wa bara la Afrika kupitia jukwaa hilo. 

    Mwaka 2017, idadi ya uagizaji wa kahawa kutoka nje ya China ilifikia tani laki 1, hivyo wafanyabiashara wa kahawa wa nchi mbalimbali wanataka kupata soko kubwa la China. Mwaka huu, maduka ya kahawa ya Kenya JAVA yameingia katika soko la China, hivyo wafanyabiashara wengine wa nchi hiyo pia wameona fursa ya kibiashara nchini China. Mkuu wa shirika la kahawa la Kenya litakaloshiriki katika Maonesho ya kwanza ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China CIIE, Bibi Fridah Mbaya amesema, makampuni ya Kenya yanatilia maanani fursa hiyo ya ushiriki wa maonesho hayo, ambayo itasaidia kuinua sifa za bidhaa za nchi hiyo. Anasema,

    "Kupitia maonesho ya CIIE, soko la China litafungua mlango kwa makampuni ya Kenya. Nataka kahawa yetu iweze kuingia katika soko la China na kushindana na kahawa za nchi nyingine. Nina imani kuwa wachina wataipenda kahawa ya Kenya kama watu wa nchi nyingine. Kwangu mimi, hii ni fursa nzuri ya kufumbua macho. Maonesho ya CIIE ni maonesho makubwa zaidi duniani, nataka kutumia fursa hiyo kuinua sifa za bidhaa za Kenya ili kuwanufaisha wakulima na wateja. "

    Mbali na kahawa, chai pia ni nguzo nyingine ya uuzaji wa bidhaa wa Kenya. Kampuni ya chai ya Home Comforts ya Kenya pia itashiriki kwenye maonesho ya CIIE ili kutangaza chai yake. Kenya ni nchi inayouza chai kwa wingi zaidi duniani, huku China ikiwa nchi inayotumia chai kwa wingi zaidi duniani. Mzinduzi wa kampuni ya Home Comforts Bw. Brian Mchiri anataka kutafutua fursa kubwa zaidi ya soko na majukwaa mengi zaidi ili kuuza chai yake. Anasema,

    "Kama soko la nchi yoyote, hali ya soko la China ina sifa yake. Tunatakiwa kufahamu vizuri kuwa wateja wanahitaji nini. Tutatafiti soko na bidhaa kwa njia mbalimbali. Nimepata uzoefu mzuri katika soko la China. China inachukua msimamo wa wazi kwa chai inayoagiziwa kutoka nje. "

    Katika mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika hapa Beijing mwezi wa Septemba, kiongozi wa China alitangaza kuwa China imeamua kupanua uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika hasa bidhaa zisizo za maliasili, na kuziunga mkono nchi za Afrika kushiriki katika maonesho ya CIIE. Kampuni ya Centrofood ya Kenya yenye historia ya miaka 38 pia itashiriki kwenye maonesho hayo. Kechapu na jemu zinazotengenezwa na kampuni hiyo, zinauzwa katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda, Rwanda na Sudan Kusini. Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Dominic Mukubwa alipozungumzia sababu ya kulenga soko la China lililoko mbali na Kenya, amesema soko la China ni kubwa, wateja ni wengi, pia kuna majukwaa mengi ya biashara za kielektroniki. Bidhaa za kilimo za Kenya zina sifa nzuri, hivyo anataka maonesho ya CIIE kuziwezesha serikali za nchi hizo mbili kusaini makubaliano zaidi, ili kuuza bidhaa nyingi zaidi za Kenya nchini China. Hivi sasa, ametuma sampuli za kilo 20 huko Shanghai. Anasema.

    "Maonesho ya CIIE yataniwezesha kuona mambo mengi zaidi, ambayo ni fursa nzuri zaidi kwa makampuni ya Kenya. Makampuni yetu yanatakiwa kuonesha bidhaa zetu nzuri kwa wachina. Naona soko la majukwaa ya biashara za kielektroniki ya China lina mustakabali mzuri, ambayo yatakuwa njia nzuri kwetu kuuza bidhaa. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako