• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Moyo wa mageuzi kuleta ajabu kubwa zaidi ya China

  (GMT+08:00) 2018-10-26 18:28:53

  Katika miaka 40 iliyopita tangu China itekeleze sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, uchumi wa nchi hiyo umeinuliwa hadi nafasi ya pili duniani, ambapo ukubwa wa viwanda vya utengenezaji umeshika nafasi ya kwanza duniani, na watu zaidi ya milioni 700 wamefanikiwa kuondokana na umaskini. Mabadiliko hayo yanaitwa "Ajabu ya China" na wasomi wa nchi za magharibi. Kwa kukabiliana na hali ya kimataifa inayobadilika na changamoto ya mabadiliko ya mtindo wa maendeleo ya ndani, China itaweza kutimiza ajabu mpya au la? Ukaguzi wa rais Xi Jinping wa China mkoani Guangdong umetupa jibu thabiti kuwa mageuzi ya China hayatasimamishwa, ufunguaji mlango pia utazidishwa, na China itakuwa na ajabu mpya itakayoshangaza dunia.

  Mji wa Shenzhen ulikuwa kituo muhimu cha ziara ya rais Xi Jinping wa China mkoani Guangdong. Maendeleo ya mji huo katika nusu ya kwanza ya mwaka huu yamevunja hoja kwamba uchumi wa China unadidimia. Takwimu za serikali zimeonesha kuwa, katika miezi minane ya mwanzo ya mwaka huu, idadi ya kampuni mpya zinazowekezwa na mitaji ya kigeni mjini humo imefikia 9,724, ambayo imeongezeka kwa asilimia 186.25 ikilinganishwa na ya mwaka jana. "Wimbi la kuondoka kwa mitaji ya kigeni" lililotangazwa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi halijatimia, kinyume chake ni kwamba kwa kutegemea nguvu bora ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, mnyororo wa utoaji, mnyororo wa viwanda, rasilimali ya watu na mazingira bora ya biashara pamoja na uzinduzi wa daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macau, ustawi wa eneo la Dawan la Guangdong, Hong Kong na Macau, mji huo unaendelea kuwa chaguo la kwanza la wafanyabiashara wageni.

  Ajabu mpya ya maendeleo ya Shenzhen ni taswira ya China kuelekea maendeleo ya sifa ya juu. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, China imekuwa nchi inayopokea uwekezaji mwingi zaidi kutoka nje duniani, ambao umeongezeka kwa asilimia 6 ikilinganishwa na wa mwaka jana, na kuzidi bingwa wa mwaka jana, ambaye alikuwa ni Marekani.

  Katika miaka kadhaa iliyopita, mchango wa China kwa ukuaji wa uchumi wa dunia umezidi asilimia 30, huku mchango wake kwa kazi ya kupunguza umaskini ya dunia ukizidi asilimia 70. China imekuwa nguvu muhimu ya maendeleo ya uchumi wa dunia na mfumo wa utawala wa dunia, na China yenye moyo wa mageuzi na ufunguaji mlango itaendelea kuleta fursa nyingi zaidi za maendeleo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako