• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni zahimizwa kushiriki kwenye mashindano ya kampuni 100 bora

    (GMT+08:00) 2018-10-26 19:16:12

    Mwenyekiti wa Bodi ya Mwananchi Communications Limited nchini Tanzania (MCL) Bw Leonard Mususa amezitaka kampuni nyingi zaidi kujitokeza na kushiriki mashindano ya kampuni 100 bora za kati (Top 100).

    Amesema hayo katika hafla ya fainali mjini Dar es salaam ikiwa ni mwaka wa nane tangu yalipoanzishwa mwaka 2011.

    Mususa amesema mashindano hayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara wa kati kukutana na kubadilishana mawazo ya namna ya kukuza biashara zao.

    Wakati huo huo wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara nchini Tanzania wamesema kupungua kwa wanunuzi wa zao hilo ni miongoni mwa sababu za kushuka kwa bei mwaka huu.

    Hata hivyo, wakulima hao wamegoma kuuza korosho zao kwenye minada mitatu ya kwanza msimu huu kutokana na kushuka kwa bei ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka jana. Wakati mwaka jana kulikuwa na kampuni 60 zilizokuwa zinanunua korosho, hadi sasa ni kampuni 35 pekee zilizojitokeza kununua zao hilo lakini wakulima wamegoma kuuza kutokana na bei ndogo iliyotangazwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako