• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Japan

    (GMT+08:00) 2018-10-26 20:26:34

    Rais Xi Jinping wa China hapa Beijing amekutana na waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe ambaye yuko ziarani nchini China.

    Rais Xi amempongeza Bw. Abe kwa kuonesha nia ya kuboresha na kuendeleza uhusiano kati ya China na Japan na kusema, nchi hizo mbili ni majirani, na maslahi zao zinaungana. Zikiwa nchi muhimu za kiuchumi duniani, ukuaji wa uhusiano kati ya nchi hizo unaendana na maslahi ya msingi ya watu wa pande hizo mbili, ambao pia ni matarajio ya kanda hiyo na jumuiya ya kimataifa.

    Bw. Abe amesema, anafurahi kufanya ziara nchini China wakati wa maadhimisho ya miaka 40 tangu Japan na China zisaini makubaliano ya urafiki na amani kati ya pande mbili. Amezitaka nchi hizo zianzishe zama mpya ya uhusiano kati ya pande mbili unaobadilika kutoka ushindani kuwa uratibu kupitia ziara yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako