• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya waziri mkuu wa Japan yaonyesha mambo muhimu ya ushirikiano kati ya China na Japan

    (GMT+08:00) 2018-10-27 18:33:07

    Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amefanya ziara nchini China kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 27 Oktoba, ambayo ni ziara ya kwanza kwa waziri mkuu wa Japan katika miaka 7 iliyopita.

    Chini ya uongozi wa pamoja wa rais Xi Jinping wa China na viongozi wa Japan, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umerudi kwenye njia sahihi, na uko katika mwanzo mpya. Maendeleo yafuatayo yanaamuliwa na namna ya pande mbili kupanua ushirikiano.

    Kwa mujibu wa ajenda ya ziara ya waziri mkuu wa Japan, ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika siku za baadaye utatokana na mambo matatu ambayo ni kuimarisha msingi wa uaminifu wa kisiasa kati ya pande mbili, kupanua sekta za kunufaishana, na kuondoa tofauti ya maingiliano ya watu kati ya pande mbili.

    Katika siku za baadaye, kama nchi hizo mbili zinaweza kufanya juhudi katika mambo hayo matatu, China na Japan zitakuwa nguvu muhimu katika maendeleo ya Asia na dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako