• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manyika Jr alamba dili nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2018-10-29 10:39:58

    Aliyekuwa mlinda mlango wa timu ya Singida United ya nchini Tanzania, Peter Manyika Jr, amejiunga na klabu ya KCB ya Kenya inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo.

    Akiongea na kituo cha televisheni cha East Afrika baba mzazi wa Manyika Jr, Peter Manyika amesema kijana wake amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu Oktoba 25, 2018. Manyika amejiunga na klabu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya kuondoka Singida United kutokana na kushindwa kulipwa stahiki zake ikiwemo malipo ya usajili na mishahara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako