• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zaidi ya aina 5000 za bidhaa zitaoneshwa katika Maonesho ya kwanza ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China

  (GMT+08:00) 2018-10-29 18:11:34

  Maonesho ya kwanza ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China yatafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 10 Novemba, mjini Shanghai. Mjumbe wa mazungumzo ya biashara ya kimataifa wa Wizara ya biashara ya China Bw. Fu Ziying ameeleza kuwa, rais Xi Jinping wa China atahudhuria sherehe ya ufunguzi na kuandaa shughuli zinazohusika.

  Mjumbe wa mazungumzo ya biashara ya kimataifa wa Wizara ya biashara ya China Bw. Fu Ziying ameeleza kuwa, maonesho hayo yamependekezwa na kutangazwa duniani na rais Xi Jinping wa China, ambaye pia atahudhuria ufunguzi wa maonesho hayo na kufanya shughuli zinazohusika. Bw. Fu anasema:

  "Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje ya China yatafanyika kati ya tarehe 5 na 10 Novemba mjini Shanghai. Rais Xi Jinping wa China atahudhuria sherehe ya ufunguzi pamoja na shughuli zinazohusika. Maonesho hayo yatahudhuriwa na wanasiasa kutoka nchi na sehemu 150, wajumbe wa sekta ya viwanda na biashara pamoja na wakuu wa mashirika ya kimataifa.. Rais Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan wataandaa tafrija ya kuwakaribisha wageni; pia atahudhuria na kuhutubia sherehe ya ufunguzi tarehe 5 asubuhi na kutembelea Jumba la Maonesho la Kimataifa. Wakati wa maonesho hayo, rais Xi pia atakutana na viongozi wa serikali za nchi mbalimbali."

  Pia ameeleza kuwa, hayo ni maonesho makubwa ya kwanza ya kitaifa yaliyo na kauli mbiu ya uagizaji wa bidhaa duniani, ambayo yanahusisha sehemu mbili zikiwemo maonesho pamoja na baraza, ambapo nchi 82 na mashirika matatu ya kimataifa yataweka majukwaa ili kuonesha sura ya nchi, mafanikio kuhusu maendeleo ya kiuchumi na kibiashara na bidhaa zenye umaalumu wao. Bw. Fu anasema:

  "Kwenye maonesho hayo, nchi 12 zikiwemo Indonesia, Vietnam, Pakistan, Afrika Kusini, Misri, Russia, Uingereza, Hungary, Ujerumani, Canada, Brazil na Mexico ziitaandaa majumba yenye umaalumu wa nchi zao. China ikiwa nchi mwenyeji wa maonesho hayo itakuwa na jumba la China ambalo ndani yake yatakuwepo majukwaa ya Hongkong, Macau na Taiwan, yatakayoonesha maendeleo makubwa yaliyopatikana katika mchakato wa mageuzi na ufunguaji mlango nchini China, pamoja na fursa mpya zinazotokana na maendeleo ya China na kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa dunia."

  Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Bingnan ameeleza kuwa, wanachama wa kundi la G20, nchi wanachama wa BRICS, nchi wanachama wa Shirika la ushirikiano wa Shanghai, pamoja na nchi zaidi ya 50 zinazojiunga na "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na nchi zaidi ya 30 zilizoko nyuma kiuchumi duniani zitashiriki kwenye maonesho hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako