• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ndege ya Indonesia iliyobeba abiria 189 yaanguka baharini

  (GMT+08:00) 2018-10-29 19:52:55

  Idara ya uokoaji ya taifa ya Indonesia imesema, ndege ya shirika la ndege la Simba iliyokuwa na abiria 189 imeanguka baharini baada ya kuondoka Jakarta mapema leo.

  Akizungumza na waandishi wa habari, mtendaji wa idara hiyo amesema ndege hiyo iliondoka saa 12 na dakika 20 asubuhi Jakarta na kwenda Pangkal Pinang mkoani Banka Belitung, lakini ilipoteza mawasiliano dakika 13 baada ya kupaa.

  Hivi sasa imethibishwa kuwa ndege hiyo imeanguka baharini na kazi ya uokoaji inaendelea.

  Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo amesema, China inatoa salamu za rambirambi kwa ndugu na marafiki wa watu waliofariki kwenye ajali ya kuanguka kwa ndege hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako