• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Muungano wa utafiti wa Afrika wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" waanzishwa

  (GMT+08:00) 2018-10-29 19:53:39

  Muungano wa utafitu wa Afrika wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" umeanzishwa huko Guangzhou, China, ambapo umefanya kongamano la kwanza la kimataifa.

  Muungano huo umeundwa na chuo kikuu cha lugha za kigeni na biashara ya nje cha Guangdong, shirikisho la kibiashara la Afrika la Guangzhou na taasisi nyingine 34 ya kimataifa. Miongoni mwa taasisi hizo, 16 zinatoka Afrika, 2 zinatoka Ulaya.

  Mwenyekiti wa baraza la kwanza la muungano huo ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa Afrika ya chuo kikuu cha lugha za kigeni na biashara ya nje cha Guangdong Bw. Fu Lang amesema kuwa, dunia ya sasa inakabiliwa masuala mengi makuu na changamoto kubwa, China na Afrika zinapaswa kuimarisha msingi wa ushirikiano kati yao, kufanya juhudi kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, ili kuchangia amani na maendeleo ya dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako