• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonesho ya ajira ya KCETA yafanyika jijini Nairobi

  (GMT+08:00) 2018-10-30 08:58:47

  Nafasi za ajira zaidi ya 1,000 zimetolewa na makampuni ya China yanayoendesha shughuli mbalimbali nchini Kenya kufuatia kuanzishwa kwa maonesho ya kwanza ya ajira ya Chama cha Kiuchumi na Biashara kati ya Kenya na China (KCETA),ya liyondaliwa jana katika jumba la mikutano la KICC jijini Nairobi.

  Vijana wanaotafuta kazi,ikiwa ni pamoja na wale waliofuzu kutoka vyuo vikuu na wenye uzoefu katika taaluma mbalimbali walifurika katika vibanda vya maonesho ya ajira huku makampuni ya China zaidi ya 50 yakitangaza nafasi za ajira.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo ,Mkurugenzi wa masuala ya Asia na Australasia ,Balozi Christopher Chika aliyapongeza makampuni ya China kwa kuimarisha mahusiano ya nchi hizo mbili kupitia utoaji wa fursa za ajira.

  "Ningependa kusema kuwa maonesho haya yanatokea wakati ambapo kuna wasiwasi mwingi kuhusu wachina nchini Kenya na kote barani Afrika.Habari nyingi ni za uongo na za kupotosha.China inakuja kwenye sura ya dunia kwa uzuri na malengo chanya, na tunaona matokeo ya kujihusisha na wachina barani Afrika na katika nchi yetu.SGR ndio maarufu zaidi lakini China imefanya miradi mingi,hayo yanaelezwa na uwepo wa makampuni haya hapa.Uhusiano wetu na China ni ule wa kimkakati na uko thabiti.

  Aidha Balozi Chika alisema kuwa maonyesho ya Kimataifa ya Bidhaa za nje ya China yatakayoandaliwa mapema mwezi ujao mjini Shanghai China,ambayo yatahudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta ,yatakuwa jukwaa kubwa la kimataifa la kuimarisha biashara mahusiano baina ya nchi.

  Kaimu Balozi wa China nchini Kenya,Bw Li Xuhang,alisema makampuni ya China yanatarajia kuajiri wakenya waliofuzu katika taaluma mbalimbali.

  Alitoa wito kwa wanafunzi na wakenya kukimbilia fursa hizo za ajira.

  "Leo tuna jukwaa zuri sana la wakenya wote kupata kazi nzuri.Makampuni ya China yamechagua kuwa ya ndani zaidi,kwa sababu tunajua kuwa wafanyakazi wa Kenya ni wakakamavu,na wanaona mbali.Wao ndio wajenzi wa muujiza wa Kenya"

  Akizungumza kwa niaba ya makampuni yote yaliyoshiriki kwenye maonesho hayo,Mwenyekiti wa Chama cha Uchumi na Biashara kati ya Kenya na China (KCETA),ambaye pia ni naibu rais wa kampuni ya Power China,Bw Wang Yantao, alisema makampuni ya China yamesisitiza kuhusu umuhimu wa kutoa nafasi za ajira kwa wenyeji,ambayo ni sehemu kubwa ya majukumu ya kijamii ya kampuni hizo.

  "Nina furaha kuona kwamba vijana wengi wamejitokeza katika maonesho haya ya ajira,jukwaa mbalo linatoa fursa ya kipekee ya ushirikiano kati ya waajiri na wanaotafuta kazi.Hapa tuna zaidi ya vibanda 60 na tunatoa fursa za ajira kutoka 100 hadi 1,000.Ni matumaini yangu maonesho haya yatazaa matunda na yatafaidi pande zote-waajiri na wanaotafuta kazi"

  Kennedy Ngure ni mmoja wa vijana waliojitokeza katika maonesho haya.Ana imani kwamba ataajiriwa na mojawapo ya kampuni za China zilizotangaza nafasi za kazi katika maonesho haya.

  Baadhi ya makampuni makubwa yanayoshiriki maonesho haya ni pamoja na China Road and Bridge Corporation,SinoHydro Corporation,Huawei Technologies, AVIC International,miongoni mwa mengine.

  KCETA ni shirika lisilo la faida,lenye kampuni 97 wanachama.Chama cha KCETA kinalenga kuimarisha ushirikiano wa biashara kati ya wakenya na watu wa China na kuboresha mabadilishano ya utamaduni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako