Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa, viwanda vya watu binafsi vimechagia sana uchumi wa China na vina mustakabali mzuri.
Rais Xi amesema hayo hivi karibuni alipofanya ukaguzi katika mkoa wa Guangdong. Amesema uvumbuzi, utengenezaji na uanzishaji wa biashara wa China hauwezi kufanyika bila ya viwanda vidogo na vya kati, na kuzitaka kamati za chama na serikali katika ngazi mbalimbali kuweka mazingira mazuri kwa viwanda hivyo. Pia ana matumaini kuwa viwanda hivyo vitaimarisha uvumbuzi kwa kujitegemea na kupata maendeleo mapya.
Rais Xi amesema, viwanda vya watu binafsi na viwanda vidogo na vya kati ambavyo vina uwezo wa kutoa uamuzi kwa haraka, na kuwa na utaratibu wenye unyumbufu wa uendeshaji, ni nguvu muhimu katika kuhimiza uvumbuzi wa sayansi na teknolojia nchini China.
Kauli ya rais Xi Jinping si kama tu imeonesha uaminifu wa kisiasa na uungaji mkono wa kisera kwa viwanda vya watu binafsi,bali pia ni msukumo muhimu kwa kuhimiza maendeleo ya siku za baadae na uvumbuzi endelevu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |