• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushirikiano wa kilimo kati ya China na Afrika wajadiliwa kwenye Umoja wa Mataifa

  (GMT+08:00) 2018-10-30 20:01:47

  Miradi ya kilimo inayofanywa na China imesaidia kuongezeka kwa uzalishaji wa chakula na kipato kwa wakulima wadogo katika nchi za Guinea-Bissau na Msumbiji.

  Katika ziara yake ya kwanza kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Mamlaka ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa ya China (CIDCA) iliungana na Ujumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuonyesha matokeo ya uhusiano wa China na Guinea – Bissau na Msumbiji katika maendeleo ya kilimo.

  Miradi hiyo miwili katika nchi za Afrika inawahusisha wakulima wadogo na uzoefu wa China, teknolojia, na mfumo wa soko jumuishi ili kuboresha uzalishaji wa chakula.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako