• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Dk Mengi kuanzisha kiwanda cha kutengeza simu

    (GMT+08:00) 2018-10-31 19:25:32
    Kampuni ya IPP Touchmate Ltd inatarajia kuanzisha kiwanda cha kutengeneza simu za mkononi za kisasa na za bei nafuu.

    Sambamba na simu hizo,kiwanda hicho pia kinatarajia kutengeza vifaa mbalimbali vya kielektroniki kwa matumizi ya nyumbani.

    Kiwanda hichi kitakachokuwa cha kwanza Afrika Mashariki,kitajengwa eneo la Mikocheni,jijini Dar es Salaam,na uwekezaji wake unakadiriwa kuwa Sh11.5bilioni na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha simu za mkononi 1,200 kwa siku,kuajiri watu zaidi ya 2,000 na watu wenye ulemavu watapewa kipaumbele.

    Mwenyekiti Mtendaji wa IPP,Dk Reginald Mengi,aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa kuitangaza kampuni hiyo na kueleza kuwa lengo ni kuunga mkono serikali ya awamu ya tano kuhusu Tanzania ya viwanda.

    Dk Mengi alisema IPP Touchmate Ltd imejiandaa kukabiliana na ushindani wa kampuni nyingine zinazoingiza bidhaa nyingine kama hizo barani Afrika..

    Aidha alisema kampuni hiyo iatatengeza simu ambazo zina uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja,pamoja na kutumika kuchajia simu nyingine,zikiwa ni maalumu kwa mazingira yenye matatizo ya umeme hususan vijijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako