• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuhimiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusukuma mbele mchakato wa utatuzi wa kisiasa kuhusu masuala nyeti ya kikanda

    (GMT+08:00) 2018-10-31 19:31:07

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo hapa Beijing amesema, kuanzia tarehe Mosi Novemba, China itakuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Amesema kwa sasa China inafanya mazungumzo na nchi wanachama wengine wa Baraza hilo kuhusu mpango wa kazi wa mwezi Novemba, na italihimiza Baraza hilo kusukuma mbele mchakato wa utatuzi wa kisiasa wa masuala nyeti ya kikanda. Pia amesema, Baraza la Usalama litafanya mikutano kadhaa kujadili masuala kuhusu hali ya Syria, Libya, Iraq, Lebanon, Mashariki ya Kati, Bosnia na Herzegovina na sehemu ya Sahel.

    Amesema China italihimiza Baraza hilo kufuata kanuni ya katiba ya Umoja wa Mataifa, kushikilia haki, mshikamano na ushirikiano, kuchukua hatua zenye ufanisi, kusukuma mbele mchakato wa utatuzi wa kisiasa kuhusu masuala nyeti ya kikanda, na kufanya kazi kubwa katika kulinda amani na usalama wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako