• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Reli ya SGR imesafirisha abiria milioni 2 nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2018-11-01 09:29:35

  Naibu meneja mkuu wa Kampuni ya operesheni ya reli ya Africa Star inayosimamia uendeshaji wa treni ya abiria ya reli ya SGR Bw. Li Jianfeng, amesema reli ya SGR ya Kenya imesafirisha abiria zaidi ya milioni 2 kati ya Nairobi na Mombasa tangu ilipozinduliwa mwezi wa Mei mwaka jana.

  Bw. Li amesema hayo wakati wabunge, wasomi na wanahabari wa Kenya wakitembelea kituo kikuu cha reli ya SGR cha Nairobi ili kufahamu jinsi ya kuendesha huduma za usafirishaji wa watu na mizigo.

  Bw. Li pia amesema, reli hiyo imesifiwa na abiria wa ndani na nje kutokana na usalama, urahisi na huduma za wateja zilizoboreshwa.

  Ameongeza kuwa hadi kufikia Oktoba 28, abiria zaidi ya milioni 2, walikuwa wamesafiri kwa reli hiyo, na kiwango cha viti vilivyokaliwa kimefikia asilimia 97.2.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako