• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wafurahia wito wa kusimamisha uhasama nchini Yemen

    (GMT+08:00) 2018-11-01 09:40:31

    Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Bw Martin Griffiths amefurahia wito wa kurejesha mchakato wa kisiasa na kusimamisha uhasama nchini humo.

    Ametoa taarifa akisema njia ya kijeshi haiwezi kuondoa mapambano, na kuwa ataendelea kushirikiana na pande zote na kuchukua hatua za kiutendaji, ili kuwaepusha wananchi wa Yemen kuathiriwa na mapambano, na kutatua msukosuko wa kisiasa, kiusalama na kibinadamu nchini humo.

    Ameongeza kuwa atahimiza pande husika zitumie fursa ya kurejesha mazungumzo ili kufikia makubaliano ya kisiasa na kujenga uaminifu, hasa katika kuongeza uwezo wa Benki kuu ya Yemen, kubadilishana wafungwa na kufungua tena uwanja wa ndege wa Sana'a.

    Wakati huo huo, Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa WFP limesema watu zaidi ya milioni 8.4 wa Yemen wanakabiliwa na balaa la njaa. Msemaji mkuu wa shirika hilo mjini Geneva Bw Herve Verhoosel amesema kama watu hao hawatapewa msaada wa chakula watakabiliwa na hali ya dharura.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako