• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar: Tamasha la tano la kibiashara kufanyika Zanzibar

  (GMT+08:00) 2018-11-01 19:01:27
  Visiwa vya Zanzibar vitashuhudia shughuli isiyokuwa ya kawaida kwa kuandaa tamsha la tano la kibiashara kuanzi hiyo kesho tarehe mbili hadi 15 Novemba. Hafla hii itatoa fursa mwafaka kwa wafanyabiashra kutoka sehemu mbalimbali kunadi na kuuza biashara zao. Kwa mujibu wa Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar Balozi Amina Salum Ali, tamasha hili litavutia zaidi ya wafanyibiashara 250 kutoka ndani nan je ya nchi.

  Waziri amewaomba wafanyabiashara wote kuja na bidhaa zenye ubora unaostahili ili kwenye tamasha hilo litakalofanyika kwenye viwanja vya Maisara. Aidha fursa hii itasaidia sana kuiuza Zanzibar kwa mataifa ya nje kama taifa lenye kivutio kwa utalii hivyo basi kuongeza pato lake. Wazanzibar wamehimizwa kukuza biashara yao na kuthamini bidhaa zinazozalishwa nchini mwao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako