Kupitia mwakilishi wake nchini Tanzania Stephen Kargbo, unido imesema kuwa mradi huo utawawezesha wazalishaji kuja na bidhaa za ubora wa juu na unaostahili kwenye masoko ya utalii. Mradi huu utakaofadhiliwa na serikali ya Uswisi, unalenga kuzisaidia kampuni za wazawa kufikia kiwango cha ubora wa bidhaa cha kimataifa kinachostahili, ambacho ni ISO 22000.
Naye mshauri wa kitaifa wa mradi huo kutoka Unido Vedastus Timothy, alisema watalii wanataka kutumia bidhaa zilizozalishwa na kusindikwa nichi Tanzania, bora tu ziwe salama na zenye ubora wa kimataifa. Wasindikaji waliopewa mafunzo wameombwa kuwafunza wenzao ili kusindika bidhaa kwa viwango vya ubora wa kikanda, kitaifa na kimataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |