• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa: Wakimbizi na wahamiaji kupewa mafunzo ya ujasiriamali.

    (GMT+08:00) 2018-11-01 19:02:46
    Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa yamezindua mwongozo wa sera mpya kwa nchi zinazohifadhi wakimbizi na wahamiaji, wadau wa maendeleo na washirika wa kibinadamu, utakaosaidia kujenga fursa za kiuchumi kwa wahamiaji na wakimbizi. Mwongozo wa sera hiyo mpya unaoyahusisha shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM na kamati ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo na biashara UNCTAD , umezinduliwa kwenye kongamano la la kimataifa la uwekezaji linalofanyika mjini Geneva Uswis.

    Mashirika hayo yanasema moja ya fursa kubwa ya kufanikisha azma hiyo ni ujasiriamali ambao una uwezo wa kuweka mazingira ya faida kwa pande zote, yaani kwa wakimbizi na wahamiaji na nchi zinazowahifadhi.

    Kwa mujibu wa mashirika hayo, sera hiyo mpya inatoa mwongozo kwa vitendo kwa nchi zinazohifadhi wahamiaji na wakimbizi , wadau wa maendeleo na wa misaada ya kibinadamu, wa jinsi gani ya kuhakikisha kwamba wakimbizi na wahamiaji wanatumia ujuzi na uwezo walionao kujenga maisha yao na wakati huohuo kuchangia katika jamii zinazowahifandi na uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako