• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Pakistan

    (GMT+08:00) 2018-11-02 19:22:54

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri mkuu wa Pakistan Imran Khan, na kumkaribisha waziri mkuu huyo kuhudhuria maonyesho ya kwanza ya bidhaa za kimataifa ya China.

    Rais Xi amesema, China siku zote inatoa kipaumbele kwa Pakistan katika mambo yake ya kidiplomasia, kuunga mkono Pakistan kulinda uhuru, mamlaka na ukamilifu wa ardhi, na kuunga mkono serikali mpya ya Pakistan kutawala nchi bila matatizo na kusukuma mbele ujenzi wa taifa. Pia amesema anapenda kushirikiana na Bw. Imran Khan kufanya juhudi kuimarisha uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimakakati kati ya China na Pakistan, kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa China na Pakistan iwe karibu zaidi.

    Bw. Imran Khan amesema Pakistan inapongeza mafanikio ya maendeleo ya China, na inatumai kujifunza kutoka China katika maendeleo, kuwasaidia umaskini na mapambano dhidi ya ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako