• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IAEA yatarajia kuendelea kupanua ushirikiano na China

    (GMT+08:00) 2018-11-02 19:41:53

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA Bw. Yukiya Amano amesema, shirika hilo linatarajia kuendelea kupanua ushirikiano na China katika sekta mbalimbali.

    Bw. Amano amesema hayo alipokutana na balozi wa kudumu wa China katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa huko Vienna Bw. Wang Qun. Bw. Amano amesifu mafanikio yaliyopatikana na China katika kuendeleza mambo ya nishati ya kinyuklia, mchango uliotolewa na China katika kusukuma mbele usalama wa nyuklia duniani, na umuhimu na ushawishi wa China katika utatuzi wa masuala ya nyuklia kwenye peninsula ya Korea na Iran.

    Kwa upande wake, Bw. Wang amesema, katika miaka 10 iliyopita, ushirikiano kati ya China na IAEA katika nishati ya nyuklia, usalama wa kinyuklia, matumizi ya teknolojia ya kinyuklia, na ushirikiano wa teknolojia umepata mafanikio makubwa. Amesema China inatarajia kushirikiana na shirika hilo zaidi kuhimiza matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia na kuzuia kuenea kwa silaha za nyuklia ili kujenga dunia nzuri zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako