• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya Zimbabwe yaeleza matarajio makubwa kwa Maonesho ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China

  (GMT+08:00) 2018-11-03 17:04:10

  Mkurugenzi masoko wa kampuni ya Procitru ya Zimbabwe Bw. Tatenda Mukazi ameeleza matarajio makubwa kuhusu Maonesho ya kwanza ya uagizaji bidhaa ya China yatakayofunguliwa tarehe 5 huko Shanghai.

  Akiongea na mwandishi wetu wa habari kabla ya kufunga safari ya kuja China, Bw. Mukazi amesema, kampuni ya Procitru inashughulikia uuzaji wa mazao ya kilimo ya Zimbabwe kwa nje. Kwenye maonesho hayo, kampuni hiyo itatangaza mazao ya kilimo ya Zimbabwe kwa wanunuzi kutoka China na sehemu mbalimbali duniani kwa njia ya video.

  Ingawa kampuni hiyo ilianzishwa mwaka huu tu, lakini imeuza tani 300 za maboga na matunda ya Zimbabwe nchini Uholanzi. Hivi sasa wanunuzi wake wanatoka Ulaya, Afrika Kusini na Mashariki ya Kati. Bw. Mukazi amesema, atakwenda Shanghai kushiriki Maoneshao ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China akiwa na matarajio makubwa. Anasema,

  "Tunatarajia kutimiza lengo la kuuza zaidi ya tani 500 za mazao ya kilimo ya Zimbabwe mwaka 2019. Tukizingatia idadi kubwa ya watu wa China, na idadi ya uzalishaji wa mazao yetu, tutatambua hii ni fursa nzuri kwetu."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako