• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kamati ya kuhimiza usafirishaji nje ya Kenya yasema Kenya itanufaika na mafanikio ya maendeleo ya uchumi wa China

  (GMT+08:00) 2018-11-03 17:42:07

  Mwenyekiti wa kamati ya kuhimiza usafirishaji nje ya Kenya Bw. Peter Biwott hivi karibuni alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, Maonesho ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China yatakayofanyika huko Shanghai, China, yamefungua njia kwa dunia nzima kuuza bidhaa kwa China, na dunia nzima itanufaika na maendeleo ya uchumi wa China.

  Akiwa kiongozi pekee kutoka nchi ya Afrika , rais Uhuru Kenyatta wa Kenya atashiriki kwenye maonesho ya kwanza ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China. Imefahamika kuwa kampuni za Kenya zitaonesha mazao ya kilimo, vyakula na sekta ya fedha kwenye maonesho hayo. Bw. Biwott anasema,

  "Mara hii tutaonesha bidhaa zinazouzwa kwenye soko la China na bidhaa zitakazosafirishwa nchini China. Tuna chai, kahawa, maharagwe ya Kenya, maua na mazao ya kilimo. Pia sekta ya fedha na sekta ya huduma zitaonekana ambazo zinaweza kufanya ushirikiano na upande wa China."

  Bw. Biwott amesema Kenya inazihimiza kampuni zake ziiuzie bidhaa China, pia inapenda kuwavutia wachina wengi zaidi kutalii nchini Kenya, na kunufaika na ongezeko la uchumi wa China. Anasema,

  "China imepata maendeleo ya kasi katika miaka 40 iliyopita, dunia nzima itanufaika na maendeleo yake, na Kenya pia. China inaagiza bidhaa kutoka Kenya, pia inaisaidia Kenya kujenga miundo mbinu ili kuongeza kipato cha wakenya. Tunapenda kuijenga Kenya kuwa nchi kubwa kama China."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako