• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Dunia nzima yaingia kwenye soko la China kwa kupitia maonesho ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China

  (GMT+08:00) 2018-11-04 16:19:46

  Maonesho ya kwanza ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China yatafunguliwa kesho mjini Shanghai, ambayo yatajenga jukwaa jipya la ushirikiano kwa zaidi ya 3,000 ya kampuni kutoka nchi na sehemu 130, na pia yatatoa fursa mpya kwa nchi mbalimbali kunufaika na maendeleo ya uchumi wa China.

  Ikilinganishwa na maonesho mengine ya uagizaji na usafirishaji wa bidhaa duniani, maonesho hayo yatakayofanyika mjini Shanghai ni maalumu, ambapo si kama tu kampuni na nchi mbalimbali zitaonekana, bali pia kutawepo na biashara ya bidhaa na biashara ya huduma, vilevile washiriki watafanya majadiliano kuhusu masuala muhimu ya kiuchumi na kibiashara duniani.

  Hivi sasa wanaviwanda na wafanyabiashara wa nchi mbalimbali wana wasiwasi na hali inayozidi kuwa mbaya kama vile kuongezeka kwa vitendo vya kujilinda kibiashara, na kupungua kwa ongezeko la uchumi. Wanatarajia kuingia kwenye soko la China kupitia maonesho hayo ya wazi. Kampuni hodari duniani zinazoshughulikia sekta ya roboti zikiwemo KUKA, ABB na FANUC zitaleta mafanikio mapya, na gari la kwanza duniani linaloweza kuruka ambalo linatengenezwa na Slovakia pia litaonekana kwenye maonesho hayo.

  China ni soko kubwa lenye watu bilioni 1.4. China imeleta fursa kubwa kwa wenzi wake wa biashara duniani, bila kujali kama nchi zilizoendelea au nchi zinazoendelea.

  Tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango miaka 40 iliyopita, si kama tu imenufaika na ufunguaji mlango, bali pia imeunga mkono ufungaji mlango bila kusita, na siku zote inaunga mkono biashara huria na kurahisisha uwekezaji. Rais Xi Jinping wa China alieleza imani kwa nyakati tofauti kwamba China itashikilia kufungua mlango kwa pande zote, na kuzikaribisha pande mbalimbali zinufaike na maendeleo ya China.

  Huduma zinazotolewa na maonesho hayo kwenye urahisi wa kupita forodhani, hakimiliki za ujuzi, fedha na uhakikisho wa kisheria, hakika zitawafanya wafanyabiashara wa nchi mbalimbali waone nia ya dhati ya China katika kufungua zaidi mlango.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako