• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli ya SGR yakaribisha abiria wake wa milioni 2

    (GMT+08:00) 2018-11-04 16:28:11

    Reli ya SGR ya Kenya imefanya sherehe ya kukukamilisha kusafirisha abiria milioni 2. Hadi tarehe 31 mwezi Oktoba, reli hiyo imeendeshwa salama kwa kilomita laki 8 na elfu 40.

    Bibi Rose Mbogo ambaye ni mwalimu wa Taasisi ya Mafunzo ya Matibabu ya Kenya anaishi mjini Mombasa, lakini mume wake Bw. Ishmael Makumi anaishi Nairobi. Bibi Rose alikuwa abiria wa milioni 2, na kupata zawadi kubwa kutoka kwa Reli ya SGR, ikiwemo cheti cha kuwa abiria wa milioni 2 kilichosainiwa na naibu mkurugenzi wa idara ya reli Bw. Philip James Mainga, kuboresha kiti chake kwa bure, na kupata huduma kwa njia kamili.

    Reli ya SGR inachukuliwa kuwa ni mradi wa karne kwa Kenya, ni mradi mkubwa wa ujenzi wa miundo mbinu tangu ipate uhuru. Reli hii inayounganisha mji mkuu wa Kenya, Nairobi na bandari kubwa kabisa katika Afrika Mashariki, Mombasa, na imetoa rahisi kubwa kwa wenyeji.

    Naibu Mkurugenzi wa idara ya reli Bw. Philip James Mainga amesema kuwa,

    "Kwa sisi sote, huu ni muda wa furaha. Tukiangalia nyuma, reli mbili zilizokuwa kufanyakazi, na katika mwaka huu, kwa mahitaji ya safari ya watu, tunaongeza reli zinazoendesha kati ya miji hiyo miwili ambalo ni jambo la ajabu sana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako