Rais Xi Jinping wa China leo tarehe 5 amehudhuria ufunguzi wa Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya Bidhaa zinazoingizwa China kutoka nje na akitoa hotuba ya "Kujenga pamoja uchumi wa dunia wa kufungua mlango ulio wa kufanya uvumbuzi na ushirikiano wa pande mbaimbali. Rais Xi akiwa kwa niaba ya serikali ya China na wananchi wake, amezikaribisha nchi, sehemu na mashirika ya kimataifa 172 pamoja na kampuni zaidi ya 3600 zinazoshiriki kwenye maonesho hayo, anawakaribisha marafiki wa nchi mbalimbali watumie vizuri fursa ya maendeleo ya China, kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, na kutimiza usitawi na maendeleo kwa pamoja. Kwenye maonesho hayo wafanyabiashara wa China na wa nchi mbalimbali wapatao zaidi ya laki nne wanatazamiwa kushiriki kwenye maonesho hayo na kufanya mazungumzo ya kuagiza bidhaa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |